BOBAN WA SIMBA SCSimba Day itafanyika sambamba na maazimisho ya Siku ya Wakulima nchini (Nanenane), kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, ambapo Wekundu hao wa Msimbazi watacheza na Simba ya Uganda.
Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kwamba maandalizi ya siku hiyo yamekamilika na wachezaji wameahidi kuonyesha viwango vya hali ya juu baada ya kukaa kambini Zanzibar kwa zaidi ya wiki moja.
“Wachezaji wetu wana ari kubwa ya ushindi ambapo wamesema katika kipindi ambacho wamekaa Zanzibar wameweza kuelewana vizuri kutokana na ugeni uliokuwepo na wapo kiushindani zaidi,”alisema Kamwaga, aliyewahi kuwa Mwandishi wa gazeti hili.
Post a Comment